Jumatatu 1 Juni 2026 - 07:05
Uwepo wa Israel Katika Ardhi yetu ni Uwepo Haram na Lazima Upingwe kwa Hali Yeyote ile

Hawza/ Mwanachama wa kambi ya “Uaminifu kwa Muqawama” katika Bunge la Lebanon alisisitiza: Kanuni ya kudumu ambayo inapaswa kuwa wazi na kuwepo mbele ya kila mtu ni kwamba; uwepo wowote wa Israel katika ardhi yetu ni uvamizi ambao lazima ukabiliwe na kupingwa bila kulegea kwa namna yoyote.

Kwamujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ali Fayyadh, mwanachama wa kambi ya “Uaminifu kwa Muqawama” katika Bunge la Lebanon, katika hafla ya kumbukumbu iliyoandaliwa na Hizbullah kwa mashahidi wawili ndugu, Abdulmunim na Ahmad Hassan Talib, huko Bir Hassan, alisisitiza:

"Kanuni ya kudumu ambayo inapaswa kuwa wazi na kuwepo mbele ya kila mtu ni kwamba; uwepo wowote wa Israel katika ardhi yetu, kwa hali yoyote ile, sura yoyote ile na kiwango chochote kile, ni uvamizi ambao lazima ukabiliwe na kupingwa bila kulegea kwa namna yoyote; hata kama mizani ya nguvu si thabiti, kwa sababu Muqawama katika hatua ya sasa ni muqawama wa kujilinda tu ambao lengo lake ni ulinzi, si kuzuia, uzuiaji hutekelezwa katika hatua ambayo ardhi tayari imekombolewa, lakini sasa Muqawama inajilinda yenyewe, uwepo wake, ardhi yake na watu wake, wajibu huu ni jambo la wazi na la kawaida, na unapaswa kuwa juu ya mijadala, migawanyiko na tofauti zote za kisiasa."

Aliongeza kuwa: "Wajibu huu hata kwa mantiki ya mazungumzo ni jambo la lazima, bali ni la msingi; kwa sababu mtu anaefanya makubaliano bila ya vyanzo vya nguvu na havitegemei, anafanya mazungumzo kwa ajili ya kushindwa, kujisalimisha na kukubali masharti ya adui."

Alisema kwamba huu dio ulikuwa udhaifu wa hatari wa mfanyaji mazungumzo wa Lebanon, ambaye kabla na wakati wa mazungumzo aliuondolea Muqawama uhalali wa kisheria, akauacha na akaingia nao katika mgongano, bila ya kuweza kufanikisha hata mafanikio madogo kabisa.

Fayyadh alisema: Wakati Lebanon imeingia moja kwa moja katika mazungumzo ya kijeshi, kusini mwa nchi hiyo kunakabiliwa na kampeni ya uharibifu na mauaji ya halaiki yenye upana mkubwa, uhalifu wa mara kwa mara unafanywa dhidi ya raia wa Lebanon, na hata watu wasiokuwa wanajeshi mjini Beirut wanalengwa, huku mwitikio wa mamlaka katika matukio haya ukiwa wa baridi, wa kimazoea, usio na maana na usio na manufaa, kana kwamba unafanywa tu kwa kutimiza wajibu wa kawaida.

Aliongeza kwamba; hakuna serikali yoyote duniani ambayo watu wake wanakabiliwa na kiwango kama hicho cha uharibifu, mauaji ya halaiki na uhalifu, halafu ikachukua msimamo wa namna hiyo, kana kwamba watu hao si wananchi wake au ni kundi la wageni ambao maumivu na mateso yao hayana umuhimu wowote.

Mwanachama huyo wa kambi ya Muqawama alisema kuwa: "Sehemu kubwa ya maoni ya umma nchini Lebanon inaiuliza Serekali: kwa nini mazungumzo yoyote na adui — kwa namna yoyote ile — hayafanywi kwa sharti la kusimamishwa kabisa na kwa ujumla mapigano? Ni nini kinachoelezea mwenendo wa mamlaka, wakati Waisraeli wanafanya kiwango cha juu kabisa cha uharibifu, mauaji na uvamizi ndani ya ardhi ya Lebanon, na Wamarekani wako katika kiwango cha juu kabisa cha upendeleo na usaliti wa jukumu lao la upatanishi?"

Aliongeza kuwa; njia ambayo mamlaka imeichukua haijatoa matokeo yoyote ya kuwalinda Walebanon wala kupunguza mateso yao.

Fayyadh aliendelea kusema: "Kwa mtazamo wa uhalisia, uwajibikaji na mbali na mantiki ya kauli za kishairi au mabishano yasiyo na maana, tunasema kuwa; ukubwa wa njama, hatari na mashinikizo haulingani na uwezo wa upande wowote kukabiliana navyo peke yake, hili linahitaji Walebanon, licha ya tofauti zao, kuunganisha uwezo na majukumu yao."

Kwa msingi huo alisema kuwa; mara nyingi wameishauri serikali ya Lebanon kutumia nafasi ya Muqawama badala ya kuipoteza, na pia kuitumia nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ni ya kweli na yenye jukumu muhimu na zito katika kusaidia watu wa Lebanon kumaliza uchokozi wa Israel na kuilazimisha kujiondoa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha